CHADEMA WAJIMWAGA KATIKA KUTANGAZA NIA TARIME



CHADEMA WAJIMWAGA KATIKA KUTANGAZA NIA TARIME


 WAKATI  zimwi la uchotwaji wa fedha za Akounti ya tegete Escorw likiendelea kikitesa Chama cha Mapinduzi CCM Chama cha Demorasia na Maendeleo CHADEMA Wilayani Tarime kimeendelea kuweka ngome na watangaza nia ya kugombea ubunge kuongezeka siku hadi siku  kufuatia kutia for a katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana.

Aidha katika mkutano wa chama hicho ambao ulifanyika juzi katika viwanja vya mpira wa miguu Serengengeti kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa kura na  ridhaa ya kuongoza halmashauri ya Mji hususani ngazi ya serikali za mitaa watangaza nia wazidi kujinadi. 

Kupitia mkutano huo Mwenezi wa Chama cha Demkorasia na Maendeleo CHADEMA Peter Chacha ambaye pia na Diwani kata ya Nyandoto  aliwapatia frusa wananchama wake kutumia nafasi hiyo kutangaza nia ya kugombea Ugunge jimbo la Tarime.

Aidha waliotangaza nia ni pamoja na  Peter Bhusene  Mkazi wa Nyamwaga wilayani hapa, Christopher Chomete ambaye ni diwani wa kata ya sabasaba, Pamoja na John Heche amabaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana  Taifa  (Bavicha) watu hao wameweza kutangaza nia na pamoja na kuendelea kutoa kuzidi kwa Wananchi kama wakifanikiwa kutapa uongozi mambo ambayo watawatekelezea  huku uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya kupitia Mwenyekiti wake  Lukas Ngoto alisema kuwa  hawatamlinda Mtu yeyote hadi pale ambapo  kamati tendaji itakapo pendekeza  mgombea mmoja na kumpitisha.

Bhusene ambaye ni mara yake ya kwanza kutangaza nia ya kugombea Ugunge kupitia CHADEMA alisema Chama chake kikimpitisha sanjari na Wananchi kumpa ridhaa ya kuongoza   atawaletea  wananchi maendeleo kupitia vipaumbele vya rasilimali zilizzopo kama vile makusanyo ya mapato ya rasilimali kutoka machimbo ya dhahabu na hifadhi ya Serengeti pamoja na ushuru nwa mipakani.


Aidha Bhusene aliongezaa kuwa endapo atafanikiwa kuwa Mbunge atahakikisha kuwaq Wananchi wake wananufaika na nrasilimali zilizopo jambo ambalo wabunge wengi hawajalitilifanya nza kuwa makusanyo ya ushuru wa ndizi yahawezi kumaliza matatizo na kero za Wananchi wa Tarime  

“Kila mtu anawajibu wa kutangaza nia hatuwezi kuzuia mtu yeyote lakini natoa angalizo kati ya waliotangaza nia akitumia nafasi yake kuchafua viongozi wenzake au wafuasi wake tutamushughulikia kulingana na kanuni za chama” alisema Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya Tarime Lukas Ngoto.

Aaidha  Ngoto aliongeza kuwa kwa kata ambazo zinaongozwa na madiwani wa CHADEMA hakuna haja ya Mtu yeyote kupitia CHADEMA  kutangaza nia  kwani kufanya hivyo  atatumia nafasi  hiyo kuchafua kiongozi aliyepo wakati ni wa chama chake  labla Halmashauri ya Mji wa Tarime na Halmashauri ya Wilaya ambayo ni ya Vijijini itakapo tangazwa rasmi kuwa zimegawanya.


          ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,…
Powered by Blogger.