CCM Rorya wazindua Shina la Uvccm(bodaboda) na kuchoma zaidi ya kadi 100 za ukawa.

Mwenyekiti wa CCM Halmashauri ya wiliya ya Rorya Samwel Kiboye (maarufu kama namba Tatu) akiteketeza kadi zaidi  ya 100 za  Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ni katika mkutano wa hadhara wa kufungua shina na UVCCM Bodaboda katika stendi ya Utegi Wilayani Rorya Mkoani Mara.


Chama cha mapinduzi wilayani Rorya Mkoani mara kimezindua shina la Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Boda boda katika stendi  ya Utegi wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuchomwa kwa kadi zaidi ya miamoja za  umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)zilizorejeshwa na baadhi ya wanachama wa  vyama vya tofauti tofauti vya upinzani.

Akifungua shina hilo la waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda Mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Aairo aliwataka vijana hao kuzidi kudumisha  umoja wao ikiwa ni pamoja na kuondokana na suala la kutumiwa vibaya na wanasiasa kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Aaidha Mbunge huyo amesema kuwa ahadi ambayo alihaidi hapo awali itatimizwa mnamo Desemba mwaka huu ili kuwapa hamasa waendesha pikipiki hao.
“Pikipiki mbili ambazo niliahaidi kwa sasa ziko bandarini kufiki mwezi Desemba zitakuwa zimefika na nitaweza kuwakabidhi rasmi” alisema Mbunge.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Rorya Samwel Kibo(Maarufu kama namba tatu) aliwataka waendesha boda boda hao kufungua akaunti ili kuweza kutunza fedha zao katika hali ya usalama.

Aaidha Mwenyekiti huyo aliweza kutoa  laki moja kwa lengo la kuwawezesha vijana hao kufungua akaunti hiyo huku akihaidi baada ya kufunguliwa atawapatia shilingi million mbili.

“Fungueni maramoja akaunti alafu niletee taarifa nitawapa millioni mbili kwa lengo la kutunisha mfuko wenu” alisema Mwenyekiti.
Jerard Bitaris ni moja wa  waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda alisema kuwa viongozi hawana budi kuwasaidia katika kutatua changamoto zinazowakabiri ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Tunakumbwa na changamoto nyingi katika utendaji kazi wetu hivyo viongozi wazidi kutusaidia ili tuweze kujikwamua kiuchumi kwani waliwengi tunatumia pikipiki zisizokuwa zetu” alisema Jerard.
                                         ……Mwisho…


Powered by Blogger.