TTC TARIME WAHOFIA JKT WATAKA IONDOLEWE,WAZIRI KAWAMBWA ASEMA HAIWEZEKANI.
Picha ya waziri wa Elimu Nchini
Shukuru Kawambwa akiongea na wanachuo wa Chuo cha Ualimu TTC Tarime
Mkoani Mara katika ukumbi wa chuo hicho.
SERIKALI
imesema kuwa haitasitisha mafunzo ya
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa walimu
kwakuwa mafunzo hayo yanawajengea walimu ukakamavu, nidhamu na kujua
shughuli mbalimbali za uzalishaji zikiwamo za kilimo.
Akijibu
swali la Jovenal Thomas Airo mmoja kati ya wanafunzi wa chuo cha ualimu
Tarime ndani ya ukumbi wa chuoni jana lililohoji kuna manufaa gani mwalimu kwenda JKT ? kwa
madai kuwa mpango huo hauna manufaa zaidi ya walimu kufariki wakiwa JKT
kutokana na matatizo ya kiafya,
Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa alisema kuwa Mpango huo ni mzuri kwa madai kuwa hata mika ya nyuma walimu
walikwenda JKT baada ya kuhitimu mafunzo ya chuo cha ualimu.
Kawambwa
alisema kuwa mafunzo ni miezi 3 tofauti
na miaka ya nyuma ambayo yalitolewa kwa muda wa mwaka mmoja hivyo anashangaa
kuona baadhi ya wanafunzi wakiogoma na kuhofia
mazoezi ya JKT.
“Msiogope
KJT nyie miezi mitatu tu mnaogopa! Sisi tulifanya mwaka mmoja tena mimi
nilienda JKT Bulombola Kigoma ambako ndiko kunaogopwa sana kwa mazoezi makali
lakini sikuogopa istoshe mazoezi
nikuwafanya kuwa wakakamavu na nidhamu pia”alisema Kawambwa.
Waziri
huyo alisema kuwa zoezi hiilo ni jambo
zuri kuwepo nakwamba ilikuwa ni makosa
kusitishwa miaka ya nyuma kutokana na ukosefu wa fedha za uendeshaji nakwamba kwa sasa Serikali ililitazama hilo na kuona numuhimu kurejesha
mazoezi hayo.
Wakati huohuo,Waziri huyo amesema kuwa Serikali itajitahidi kuhakikisha
ina tatua changamoto zinazoikabili chuo cha ualimu Tarime yakiwamo madeni ya
wakufunzi, na ukarabati wa majengo ya chuo.
Kawambwa
alisema kuwa Serikali imejitahidi
kupunguza madeni ya walimu ambapo pia
inatarajia kujenga vyuo vya ualimu vyenye hadhi ya kisasa tofauti na
vyuo vilivyopo sasa ambavyo vimeonekana majengo yake yamepitwa na wakati
“Tunajitahidi
kutatua changamoto kwa baadhi ya vyuo
hivyo nahaidi Tarime nayo kwa baadae yatajengwa majengo ya kisasa tumeona
tuanze ujenzi kwa vyuo ambavyo
vinachangamoto kubwa zaidi ya Tarime lakini pia tumejitahidi kupunguza madeni
ya walimu yatalipwa ila nawatahadhalisha walimu ambao wameandika madeni ya
uongo’Alisema kawambwa.
Mkuu wa chuo
cha ualimu Tarime Samwel Magige alisema kuwa chuo hicho kinakabiliwa na mapungufu kadhaa
yakiwamo ya ukosefu wa watumishi,wakufunzi,Nyumba
za watumishi,uchakavu wa miundombinu,Madeni ya wazabuni hususani chakula,fedha
za rikizo kwa watumishi na kusababisha wasiende rikizo.
Magige
alisema kuwa mbali na changamoto hizo Chuo kinaendelea na ukarabati wa baadhi
ya majengo ambapo sasa wanaendelea na ujenzi
wa Mabweni ujenzi uliogharimu milioni 14 na unaendelea nakwamba chuo kina idadi
ya wanafunzi 655 na wakufunzi 40.