Makatibu wilaya CHADEMA Mkoa wa Mara wapewa pikipik
Pikipiki zikiwa katika ofisi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Musoma mjini ili kuweza kuwagawia makatibu wilaya wa chama hicho.
CHAMA cha
demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mara kimekabidhi pikipiki 8 kwa
makatibu wa wilaya mkoani hapa zenye thamani ya Millioni 16 ili
kurahisisha utendaji kazi wa chama hicho katika wilaya zao.
Makatibu waliokabidhiwa leo pikipiki hizo ofisi ya wilaya ya Musoma mjini
ni kutoka wilaya za Serengeti,Rorya,Musoma mjini, Musoma Vijijini,Bunda,Butiama,Tarime
na jimbo la Mwibara.
Katika
kukabidhi pikipiki hizo katibu wa chama cha demokrasia na Maendeleao (CHADEMA)
Ctihacha Heche, aliwataka makatibu hao wazitumie pikipiki hizo walizopewa kwa
makatibu hao wazitumie kwa ajili ya shughuli za chama.
“Pikipiki
hizi naomba tafadhari zifanye kazi za chama zisiende kusumbua vijana wetu wa bodaboda
na kutumika vibaya kwa mambo ya starehe tukibaini hilo kwa ushahidi vya
kjutosha tutachukua hatua”alisema katibu wa chadema mkoa mara,Heche.
Katibu
alizidi kusisitiza kuwa watendaji hao wasitumie vibaya vyombo hivyo vya moto
kwa ajili ya maslahi yao binafsi suala ambalo linaweza kuleta migogoro ya hapo
badae
Naye Mhazina
wa kanda mashariki Haire Tarai katika kuzindua rasmi pikipiki hizo alisema
kuwa kanda ya ziwa mashariki ina majimbo21
na majimbo hayo yameweza kupata pikipiki hizo ambazo zimeghalimu shilingi
milioni 42.
“Makao makuu
wametoa pikipiki hizi na zimeghalimu fedha kubwa nchi nzima pikipiki
zimeghalimu zaidi ya billion 2.7 kwa zaidi ya wilaya na majimbo 130 ‘’ alisema
Haire.
Kwa upande
wa makatibu hao kwa niaba yao Johness Sando wa Musoma Vijijini, alisema kuwa,
piki piki hizo zimewawezesha kuwarahisishia usafiri katika shughuli za chama.
Aidha piki
piki hizo ni moja ya utekelezaji wa mipango ya kuimalisha chama kiweze
kushiriki vyema katika chaguzi za serikali za mitaa na mkuu wa mwaka huu na mwakani.
Piki hizo
ilielezwa kuwa ni sambamba na magari yanayotarajiwa kugawiwa kila makatibu wa
mkoa yatakayo tumiwa katika shughuli za chama hicho kabla ya uchaguzi wa mwaka
kesho.
Hafla hiyo
baada ya kumalizika kuliendeshwa kikao cha ndani na makatibu hao waliopanga
mipango na maelekezo ya chama na katibu
wa mkoa huo .
-----------------------------------mwisho-------------------------------------------------