ASKOFU ALITAKA JESHI LA POLISI KUONGEZA PINGU:
Askfu wa kanisa la Abgilikana Mwita Akili Mwita akitoa hoja yake ya kuongezwa kwa pingu katika Kongamano la Jeshi la Polisi katikaUkumbi wa CMG Motel wilayani Tarime Mkoani Mara.
Askofu wa kanisa la Anglicana Dayosisi yaJimbo la
Tarime Mwita akili amelitaka jeshi
la polisi kuongeza pingu ili kurahisisha upelekaji wa Watuhumiwa
Kituoni pamoja na Mahakamani na si kuongezwa na Mitutu ya bunduki.
Kauli hiyo
ilitolewa na mchungaji huyo hivi katika
kongamano maalumu la jeshi la polisi lililoandaliwa na Jeshi la polisi chini ya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Justus Kamugisha na kufanyika katika Ukumbi wa CMG Motel huku
Mgeni Mgeni rasmi akiwa katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw:Benedict Olekuyan.
Mchungaji
huyo alisema kuwa haoni busara jeshi la polisi kungozana na bunduki kwenda kumukamata mtuhumiwa bali busara itumike
pingu ziweze kuongezeka kwa ajila yakutumika ili kufunga watuhumiwa hao.
“Serikali
ijipange kikamilifu kununua pingu za kutosha kama itaitaji Msaada na Sisi
kanisa tutachangia kiasi chochote cha fedha
ili kufanikisha zoezi hilo” alisema Mchungaji.
Hata hivyo
Mchungaji huyo alisisitiza sua la Elimu ya Usalama kupelekwa katika shule za Msingi.Sekondari na
Vyuo ili kuweza kuwajengea Uwezo wa kutambua Maana halisi ya Ulinzi na Usalama
pamoja na Ulinzi shilikishi ikiwa ni pamja na kujua jinsi ya kutoa taarifa
katika jeshi la Polisi pasipodhulika kwa mtoa taarifa huyo.
Aidha
Mchungaji huyo aliiomba Jeshi la Polisi kufanya Utafiti wa kuzunguka Mkoa wa
mara na kufahamu Tamaduni zao zinataka nini ili waweze kufanikisha vizuri suala
la ulinzi shilikishi kutoka kwa rai haouku wakitoa Elimu juu ya ulinzi
shilikishi.
Nao baadhi
ya Washiriki katika kngamano hilo walikemea sana Vitendo vya kikatili
vinavyendelea kufanyika kwa Mama na mtoto na kulitaka dawati la jinsia kufika mara kwa mara na kuonana na vingzi wa
vitongoji, Vijiji na Kata kwani wao ndo wanajua chanzo cha Migogoro.
…..Mwisho….