Rais Magufuli aisuka upya TRA. Ateua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo hii na kuanza kazi
mara moja.
Awali
nafasi hiyo ilikuwa chini ya Bw. Bernard Mchomvu ambaye bodi yake
ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa mnamo Novemba 20 mwaka 2016.
Pamoja na hayo, Prof. Florens D.A.M Luoga ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma).