Kauli ya Mbowe Baada ya Halima Mdee Kuachiwa Kwa Dhamana
Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amezungumzia sakata la
kukamatwa kwa mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye aliachiwa jana kwa
dhamana.
Mdee
alishikiliwa na jeshi la polisi kwa siku tano kufuatia amri ya
kukamatwa iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi baada ya
kudaiwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Rais John Magufuli. Mdee
alifikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kumkashfu Rais.
Akizungumza
na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoka mahakamani jana,
Mbowe alisema kuwa Mdee alieleza kuhusu hisia zake na sio vinginevyo
kuhusu agizo la Rais Magufuli kuwa wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari watakaopata ujauzito hawataruhusiwa kuendelea na masomo.
“Sisi
kama chama na kama viongozi, tunaamini kila Mtanzania awe kiongozi
asiwe kiongozi, wa chama chochote na wa dini yoyote ana haki ya kueleza
hisia zake.
"Mdee
amesomewa mashtaka ambayo sitaki kuyazungumzia, lakini utamaduni huu
mpya unaojengwa ndani ya taifa wa kuziba midomo watu wasiseme hisia zao,
utajenga chuki katika jamii. Sisi kama chama cha kupigania haki
tunaamini, kila mtu ana haki ya kueleza hisia zake.
“Halima
ni mbunge, ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha).
Kwahiyo ni kiongozi mwandamizi, sio tu wanatakiwa waseme anatakiwa
akemee. Alipokuwa anazungumza kuhusu watoto kupata mimba alikuwa
anazungumza kama mwanamke, Mbunge na Mwenyekiti wa Bawacha,” aliongeza.
Mwenyekiti
huyo wa Chadema aliongeza kuwa chama chake kitaendelea na mjadala huo
bila kujali hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yao.