Alichsema Hakimu Kuhusu Hukumu kesi ya Bob Chacha Wangwe
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele hukumu ya kesi ya kutoa taarifa
ya uongo kupitia mtandao wa Facebook, inayomkabili Bob Chacha Wangwe,
November 8,2017.
Bob
ambaye ni Mwanaharakati ni mtoto wa marehemu Chacha Wangwe, aliyewahi
kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara na Makamu Mwenyekiti wa
Chadema-Bara.
Hukumu
hiyo ilitarajiwa kusomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo
amesema ameshamaliza kuiandaa hukumu hiyo lakini anaona ni vyema
akaisoma tarehe ijayo.
“Hukumu nimeshamaliza kuiandaa kila kitu, hivyo nitaisoma November 15,2017,”.
Katika
kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 6, upande wa utetezi
ukiwa na shahidi mmoja ambaye ni mshtakiwa mwenyewe.
Awali katika ushahidi wake, Bob amedai kuwa yeye hakuandika maneno ya upotoshaji wala hajawahi kufanya hivyo.
“Mimi
nilitoa maoni yangu kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kasoro zake za
kidemokrasia kama Watanzania wengine na waangalizi wa uchaguzi huo
walivyofanya,”.
Katika
kesi hiyo namba 167, Chacha Wange anatuhumiwa kwa kosa la kuchapisha
taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.
