SIKILIZA AUDIO; WANAFAMILIA WATATU WAFA KWA KULA ASALI TARIME

Watu watatu wa familia moja wakazi wa kijiji cha Nyantira kata ya Nyansicha Wilayani hapa mkoani Mara wanadaiwa  kufariki dunia kwa kula asali.

Kaimu kamanda wa mkoa wa polisi Tarime/Rorya Sweetbert Njewike akiongea kwa njia ya simu akiwa Shirati wilayani Rorya amesema hana taarifa hiyo ofisini kwake.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyantira James Chacha amesema tukio hilo  kutokea juni 7, 8 na 9 na kuzua taharuki kijijini hapo kutokana na aina ya vifo vya wanafamilia hao watatu kufariki kwa kufuatana.

Amewataja waliofariki kuwa ni Kerato Nyangera( 70) Regina Kerato (50) na Samwel Kerato (12) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Nyantira.

Chacha amesema "juni saba tulizika mzee mzee, baada ya kumkimbiza kituo cha afya Muriba,baada ya saa 12 akafariki,tukamleta nyumbani kuzika,tulipomaliza maziko mtoto naye akawa kwenye hali mbaya, tukamkimbiza kituoni, akafa, siku tunazika akaanza mama naye akafa pia,"alisema.

Ameongeza kuwa kufariki kwa watu hao kwa mfuatano kijiji kimeingizwa na wasiwasi  kwa kuwa wazazi hao wameacha watoto wadogo.

"Wameacha watoto wanne mmoja alikuwa anamuona bado,"alisema Chacha.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Tarime Mkumbo  Odari alisema "asali kama asali haina madhara kwenye mwili wa binadamu isipokuwa pale inakuwa imechanganyikina na sumu ndipo inapoweza kuleta madhara, na hii ndiyo maana inatumiwa kama dawa, kwenye chakula kupaka kwenye mikate," alibainisha Odari.


Sunday Magacha ni diwani wa kata ya Nyansicha alisema hadi sasa chanzo cha vifo vya wanafamilia hao hakijajulikana na uchunguzi bado unaendelea ili kufahamu nini chanzo licha ya kuwa uchunguzi wa awali uliofanywa na kituo cha afya Muriba ulionyesha kuwa walikuwa wamekula sumu.

Alisema tukio hilo lilikuwa la kwanza  na la aina yake ambalo limeacha wananchi wameathirika kisaikolojia 

"Tunaomba Serikali kuwa nyepesi inapopewa taarifa isifanyike kazi haraka na wananchi wajifunze kutokana na matukio hayo na kuwa makini ili kuepuka madhara kama haya,"alisema  Magacha.

Wakazi wa kijiji cha Nyansicha walisema kuwa vifo hivyo vilikuwa vya kushitukiza kwani kwa siku tatu kuzika watu wa familia moja kimezua maswali mengi kwenye vichwa vyao huku watoto wadogo wakiachwa bila malezi yao.

"Watu zaidi ya watano walikuwa asali na huyu mee akilima kwa ndugu yake akala kisha akapeleka nyumbani kwake lakini tulishangaa kusikia kuwa yeye na mkewe na mtoto wamefariki tena kwa kufuatana, alisema  jirani familia hiyo Magabe Iroga.

                      SIKILIZA AUDIO KUHUSU TUKIO HILO
Powered by Blogger.