Angalia Picha: katika Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yalifanyika mkoa wa Mara kitaifa
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, Jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu akiongea na wanachi katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambapo kitaifa maadimisho hayo yamefanyika Mkoa wa Mara katika Wilaya ya Tarime Viwanja vya Chuo cha Ualimu TTC Tarime Mjini, kauli mbiu ya mwaka huu ni Tokomeza ndoa za utotoni ili kufikia uchumi wa viwanda. |
Baadhi ya Ngariba ambao wamepewa na mafunzo na shirika la ATFGM Masanga na kuondokana na suala zima la ukeketaji na kuanza kushona ili kujipatia kipato chao. |
Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya akikagua kazi za mikono ya akina mama ambao walikuwa ngariba baada ya kupewa elimu na shirika hilo wameondokana na suala la kukeketa watoto wa kike. |
Restuta
Mpate kutoka shirikala Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF akieleza jinsi
walivyosaidia mambinti ambao wamekumbwa na ukatili wa kijinsia hadi
wameanza kujishughulisha wenyewe.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama Anarose Nyamubi akisalimiana na Valerie Msoka katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Kike Duniani. |
Kampuni ya HUMAN CHERISHU wauzaji wa vitambaa laini PADS Wakitoa huduma katika maadhimisho hayo |
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Jukwaa la utu wa Mtoto CDF Koshuma Mtengeti katika Maadhimisho hayo. |
Waziri anatembelea vibanda. |
Antony Guninita kutoka shirika la Search for Common Ground akieleza kwa waziri Ummy jinsi shirika hilo linavyofanya kazi. |
Tunacheza kwa furaha. |
Watoto ni siku yetu leo. |
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu alipotembelea banda liloandaliwa na shirika la ATFGM Msanga akingea na baadhi ya walikuwa ngariba lakini baada ya kupewa elimu na Shirika la ATFGM Masanga na kuamua kuachana na ukeketaji sasa wanashona ili kujipatia kipato ngariba 63 tayari wamepewa elimu na kuachana na ukeketaji. |
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akitoa zawadi kwa washindi ambao walishiriki mpira wa miguu katika tamasha lilloandaliwa na shirika la Save the Children |
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akitoa zawadi kwa washindi ambao walishiriki mpira wa miguu katika tamasha lilloandaliwa na shirika la Save the Children |
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akigawa vitambaa laini Pads kutoka kampuni ya HUMAN CHERISHU PADS |
Picha ya pamoja na watoto kutoka karatu |
Burudani |
TAZAMA VIDEO WAZIRI UMMY ALICHOKISEMA KATIKA MAADHIMISHO HAYO YA KILELE CHA MTOTO WA KIKE DUNIANI .