TUHUMA ZA USHIRIKINA, ALLY YANGA AKUMBANA NA KIPIGO KIKALI KUTOKA KWA MASHABIKI MWANZA
Shabiki
maarufu wa Yanga, Ally Yanga amekutana na kipigo kikali kutoka kwa
mashabiki walioelezwa ni wa Simba wanaoiunga mkono Mbao FC.
Mashabiki
hao wa Mwanza, wamempiga Ally Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza kabla ya Yanga kuivaa Mbao FC kwenye uwanja huo, leo.
Yanga inaivaa Mbao FC kuwania kucheza fainali dhidi ya Simba ambao jana wameufunga Azam FC kwa bao 1-0 na kutinga fainali.
Mmoja
wa mashabiki wa Simba mjini Mwanza, Fred Bundala ameiambia SALEHJEMBE,
Ally Yanga alilazimisha kuingia uwanjani na kumwaga vitu ambavyo wao
waliamini ni ushirikina.
“Mwanzo
tulimueleza kistaarabu, hakusikia. Tukamsisitiza, akaanza kutoa maneno
ya kashfa, nyie watu wa Dar mna dharau sana. Tukaona acha tumkaribishe
Mwanza,” alisema.
Ally
Yanga alionekana akiwa anatema mate yenye damu baada ya kushambuliwa na
mashabiki hao ambao walionekana wengi kuliko wa Yanga.
Juzi, mashabiki wa Yanga walikesha uwanjani hapo wakiulinda uwanja huo kuhakikisha hakuna vitendo vya kishirikina.
Lakini
mashabiki wa Mbao FC walilaumu kuwa Yanga wamekuwa wakifanya
ushirikina, nao wakaongeza nguvu kuongeza ulinzi usiku wa kuamkia leo.