Mshambuliaji
wa Yanga, Amissi Tambwe, raia wa Burundi, amesema baada ya kikosi hicho
kukaa kwenye usukani wa ligi kwa sasa lengo lao lililobakia ni
kuhakikisha wanashinda kwenye mechi zao zote ili waweze kuwa mabingwa.
Yanga
wamejikusanyia pointi 56 baada ya kushuka dimbani mara 25, pointi
ambazo zinawafanya wawe juu ya timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania
Bara huku Simba wenyewe wakikamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 55.
Mshambuliaji
huyo aliyefunga mabao tisa mpaka sasa kwenye ligi, amesema kwamba kwa
muda mrefu Simba walijiaminisha kwamba wanachukua ubingwa wakasahau
kuhusu wao ambao walikuwa wanazisuka mbinu zao kimyakimya.
“Kilichobakia
kwa sasa ni kuhakikisha kwamba tunashinda kwenye mechi zetu tano
zilizobakia kwa ajili ya kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutetea
ubingwa wetu ambao tulikuwa tunaupigania kwa nguvu kubwa.
“Niwaambie
nafasi hii tuliyonayo kwa sasa ndiyo tumemaliza kila kitu kwani
hatutaki kuona tukirejea kwenye nafasi tuliyokuwa awali na nawaomba
wenzangu tushirikiane vyema katika kushinda mechi hizi zilizobakia,”
alisema Tambwe.
SOURCE: CHAMPIONI