MAYANJA: SIMBA IKO TAYARI, IWE YANGA WALETENI IWE MBAO, WALETENI TUMALIZANE NAO
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema wao wanaisubiri timu yoyote itakayotinga fainali ya Kombe la Shirikisho.
Tayari Simba imefuzu katika fainali ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza baada kuitwanga Azam FC kwa bao 1-0, jana.
Majanya amesema wanajua watacheza fainali na Yanga au Mbao FC, hivyo hawana sababu ya kuchagua mshiriki.
"Sisi kazi yetu ni kucheza soka, kikosi chetu kitajiandaa na yoyote, awe Yanga au Mbao, tunasubiri," alisema.
Msimu
uliopita katika Kombe la Shirikisho, fainali ilikuwa ni kati ya Yanga
dhidi ya Azam FC na mechi ikaisha kwa vijana wa Jangwani kubea kombe.