KAMPUNI YA TATA YAWAFADHILI WATANZANIA KWENDA NCHINI INDIA KWA MAFUNZO YA KUTENGENEZA MAGARI.
Mkuu wa Kitengo cha
Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia),
akizungumza Makao Makuu ya Kampuni hiyo Barabara ya Nyerere jijini Dar
es Salaam jana, wakati wa hafla ya kuwaaga vijana wanne wa kitanzania
ambao wanakwenda nchini India kwa mafunzo ya miezi tisa ya kutengeneza
magari. Kutoka kushoto ni viongozi wa kampuni hiyo, Sarvan Keshri na
Udayagiri Veeru.
Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia), akisisitiza jambo.
Mgeni rasmi katika
hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu
Masingi akizungumza katika hafla hiyo. Kutoka kushoto ni mmoja wa viongozi wa kampuni ya Tata, Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
Viongozi wa kampuni hiyo ukitoa zawadi ya ua kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi.
Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni
rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi
Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu,
Robert Masatu Masingi (kulia), akikabidhiwa zawadi ya picha ya tembo na
viongozi wa kampuni hiyo. Kutoka kushoto ni Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
Mama wa msichana pekee anayekwenda
kupata mafunzo hayo, Fatma Mussa Ngulangwa (kushoto), akimkabidhi binti
yake, Mariam Shamte maua ikiwa ni ishara ya kumuaga.
Fr.Lucas Wakuganda akimkabishi maua mtoto wake anayeondoka kwenda masomoni nchini humo.
Mhitimu wa mafunzo hayo, Osmund Kapinga (katikati), akiwa amewainua mikono vijana hao ikiwa ishara ya kuwaaga.
Mkufunzi wa mafunzo wa kampuni hiyo,
Oscar Mwakagenda (kushoto), akitoa maelekezo ya injini za gari
zinazofanya kazi mbele ya mgeni rasmi na uongozi wa kampuni hiyo.
Ni furaha tupu katika hafla hiyo.
Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya karakana ya mafunzo. |