DUA ZA SIMBA KWA YANGA LEO, NI ILI IIFUNGE MBAO WAFUZU KIMATAIFA
Mashabiki
wa Simba leo wana kila sababu ya kuelekeza dua zao kuomba Yanga
iwatandike Mbao FC katika mechi ya pili ya nusu fainali ya Kombe la
Shirikisho.
Simba
haijashiriki michuano ya kimataifa kwa misimu minne sasa, jambo ambalo
linaonekana ni geni kwa timu hiyo ambayo imekuwa ikifanya vema katika
hatua hiyo na kuonekana kama wawakilishi bora wa Tanzania ingawa sifa
hiyo imepokwa sasa na watani wake, Yanga.
Tayari Simba imefuzu katika fainali ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza baada kuitwanga Azam FC kwa bao 1-0, jana.
Iwapo
Yanga watashinda leo katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza, maana yake kila kitu kitabaki kuwa cha timu hizo
kongwe.
Yaani ubingwa wa Ligi Kuu Bara na ubingwa wa Kombe la shirikisho utabaki kwa Yanga na Simba.
Kwenye
Ligi Kuu Bara timu hizo ndiyo zinazofukuzana na Simba ikiwa kileleni
lakini haina uhakika sana kama itabeba ubingwa huo kwa kuwa Yanga ambao
ni watetezi wanaonekana kuwa na kasi kubwa.
Kayika
Kombe la Shirikisho, kama Yanga akiingia fainali na kukutana na Simba,
maana yake itakuwa rasmi timu hizo ndiyo wawakilishi wa Tanzania katika
michuano ya kimataifa msimu ujao.